AJALI YA NDEGE MBILI, WATU 60 WANUSURIKA

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limethibitisha kutokea kwa ajali mbili za Ndege ( muda tofauti) leo katika uwanja wa Ndege wa Kikoboga uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo zaidi ya Watu 60 kwenye Ndege zote mbili wamenusurika. TANAPA imesema Ndege ya kwanza ya Unity Air 5H-MJH aina ya Embraer 120 majira ya saa 3:40 asubuhi ikiwa na Abiria 30, Marubani wawili na Mhudumu mmoja ikitokea Zanzibar ilipata tatizo la kiufundi wakati wa kutua kiwanjani hapo lakini kwa juhudi kubwa za Marubani na Maafisa wa kiwanja hicho hakuna madhara yaliyojitokeza ambapo Abira wote, Marubani na Muhudumu mmoja wako salama na wanaendelea na ratiba yao ya Utalii hifadhini. Moja ya ndege zilizopata ajali Katika taarifa ya pili, TANAPA imethibitisha kutokea kwa ajali ya pili leoleo saa 9:30 alasiri ikihusisha Ndege ya Kampuni ya Unity Air 5H-FLM aina ya E120 ikiwa na Abiria 30, Mar...