MBEYA COMEDY FESTIVAL NA DREAM FM MSIMU WA PILI 2023, NI MAGEUZI YA SANAA NYANDA ZA JUU KUSINI

     Zikuwa zimebakia siku chache kuelekea kwenye kilele cha MBEYA STANDUP COMEDY FESTIVAL 2023, leo viongozi wa Festival hiyo wamefika kwenye kituo cha radio Dream FM kilicho katikati ya Jiji la Mbeya na kuongelea ukubwa wa tukio hilo.
      "Mkoa wa Mbeya mbali na kubarikiwa Upatikanaji wa Vyakula, Pesa na Viongozi wakubwa Kitaifa na kimataifa ambao kila wanapopita huacha mbegu na alama njema, Mbeya pia imebarikiwa kuwa na vipaji vikubwa vya Sanaa. Mbeya ina watu wenye vipaji vya kushangaza, sasa sisi tunataka hiyo siku kwakuwa ni Festival basi watu waje waone kila aina ya Sanaa japo kubwa zaidi watu watacheka saana hiyo siku." Innopresenter wa Mbeya StandUp Comedy Festival.
   Tickets zipo kila mahali yaani ulipo basi nazo zipo, usipange kukosa hii sio ya kusimuliwa.

       Mbeya StandUp Comedy Festival 2023 itafanyika kwenye ukumbi wa TUGHIMBE HALL, uliopo Mafyati Jijini Mbeya, kuanzia Saa 1:00 Jioni mpaka Saa 6:00 Usiku.
      Makampuni mbalimbali yamejitokeza kudhamini burudani hizi wakiwemo ORYX GAS, JORDAN WATER, DREAM FM, HIFADHI YA MISITU na mengine mengi.
    Wao wanasema #Munguametupakicheko😂


Comments

Popular posts from this blog

DKT. TULIA ALIVYO WEZESHA MASOMO KWA VIJANA WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU MBEYA, SONGWE NA RUVUMA.

RAIS WA IPU MH. DKT. TULIA NA RAIS WA HUNGARY WAJADILI HALI YA AMANI DUNIANI

TK MOVEMENT YAZINDULIWA DODOMA MEI 25,2024, WAZIRI NDEJEMBI AWAAGIZA WATENDAJI KUTOA USHIRIKIANO KWA VIJANA