DKT. TULIA ALIVYO WEZESHA MASOMO KWA VIJANA WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU MBEYA, SONGWE NA RUVUMA.
Vijana watano kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe na Ruvuma waliokua masomoni Nchini Nigeria Kwa ufahili wa Spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust, wamerejea Kwa mara ya Kwanza baada ya miaka sita tangu walipoondoka mwaka 2018 walipokwenda kujiunga na kidato Cha kwanza Nchini Nigeria.
Vijana hao waliotoka katika mazingira magumu ikiwemo wengine kufiwa na Wazazi wao wameanza kidato Cha kwanza mwaka 2018 na Sasa wanarejea wakiwa wamehitimu kidato cha sita na baadae kurejea Tena Nchini Nigeria kwaajili ya kujiunga na chuo Kama anavyo tueleza meneja wa taasisi ya Tulia Trust Jacqueline Boaz.
Wakiwa katika uwanja wa ndege wa Songwe Mkoani Mbeya vijana hao wamemshukuru Dkt Tulia Ackson Kwa kuwatoa sehemu ambayo walikua hawaelewi hatma ya elimu yao na Sasa wamefanikiwa kwa hatua kubwa kuhitimu kidato cha sita na kupata ufaulu Mzuri wa kwenda chuo kikuu Nchini Nigeria, huku baadhi ya walezi wakieleza maisha ya awali ya vijana hao.
Vijana hao pia waliweza Kutembelea Shule mbili za Sekondari ambazo ni Dr. Tulia Ackson Girls Secondary School na Dr. Tulia Ackson High School zilizopita Jijini Mbeya. Ambapo ndani ya Shule hizo waliweza kutoa hamasa ya kimasomo na kutoa zawadi za Daftari kwa baadhi ya Wanafunzi waliofanya Vizuri kwenye masomo yao.
Comments
Post a Comment