SMAUJATA YAFANYA UPATANISHO WA NDOA KWA WAPENDANAO JIJINI MBEYA, VITA YA UKATILI NI MAISHA.
Uongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Mbeya umefika kata ya Iganjo mtaa wa ikhanga Halmashauri ya Jiji la Mbeya
Lengo kuu la ujio wa Viongozi hao ni mra baada ya kupokea taarifa kutoka kwa msamaria mwema ambae jina lake tuna lihifadhi
Kwa Taarifa zilizo ripotiwa ni kuwa mwanaume mmoja ambae jina lake linahifadhiwa alikimbia familia na kutekeleza mama na watoto kwa Muda wa miaka mitatu, ndipo SMAUJATA ilipo amua kuvunja ukimya na kumtafuta Baba wa familia na kumpa elimu dhidi ya ukatili na ndipo alipo gundua kuwa anafanya makosa.
Mwanaume huyo baada ya Elimu kaomba Msamaha na kuto rudia Tena kukimbia familia.
Mashujaa hao katika ziara hiyo ya kutokomeza ukatili katika jamii wameongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Usajili Mkoa Asia Boniphace, Loveness Chatanda, Christophe Palange
Viongozi wa wilaya Alie pokea ugeni huo ni Mwenyekiti wa Ufuatiliaji na Utekelezaji viongozi Maiko Makunja pamoja na Shujaa ngazi ya Kata.
"Kataa Ukatili Wewe ni shujaa"
Na Wamzi Hassan
Comments
Post a Comment