BODI YA MTETEZI WA MAMA MKOA WA MBEYA WAFANYA ZIARA CHUNYA, WAFANYA KIKAO NA MKUU WA WILAYA NA KUFIKA OFISI ZA MKURUGENZI WA WILAYANI HUMO
Mwenyekiti wa Bodi Mtetezi wa Mama Mkoa wa Mbeya Ndg. Ibrahim Shermuhamed Mwakabwanga akiwa na katibu wake Bodi hiyo Ndg. Asajile Mwankina wamefanikiwa kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Simon Mayeka na kufanya utambulisho pamoja na Kikao kifupi
Aidha katika kikao hicho mambo kadha wakadha yamejadiliwa ikiwemo na somo la uzalendo pamoja na kulinda heshima ya Mkuu wa Nchi ambae ndiye Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, upande wa Bodi wameeleza dira na mpango kazi wao wa kuhakikisha Mama anapata kura za kutosha ifikapo mwaka 2025. Na katika kufanya kazi za Taasisi ni kwamba Watetezi watafanya kazi zao kijamii, kiuchumi pamoja na Siasa inayo mlenga Mama wa Taifa.
Mkuu wa wilaya amewapongeza sana Viongozi hao walio wakilisha Viongozi wengine kutoka Taasisi hiyo.
Pichani ni Katibu wa Mkoa Mtetezi wa Mama Daudi Yilanga, Katibu uhamasishaji Mkoa Sharifa Mwalukuta pamoja na Mjumbe kutoka Mbarali Angetile Bukuku.Bodi Mtetezi wa Mama pia imefika ofisi ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kusaini kitabu Cha wageni.
Ziara hiyo muhimu kwa Taasisi Mkoa wa Mbeya inaambatana na kuunda na kutafuta Mabalozi wa Taasisi ambao watajitolea katika kuhakikisha Wana yasema na kuyatangaza mazuri yote yanayo fanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakupitia wasaidizi wake ambao ni Mkuu wa Mkoa pamoja na Wakuu wa Wilaya.
Mkoa wa Mbeya hakuna kilicho simama kazi zinaendelea na tuna jambo letu 2025 ni kura za kutosha kwa *S.S.HMama anatosha tumaini la Watanzania wote
Comments
Post a Comment