SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI, DKT. GWAJIMA ASIMAMA NA MASHUJAA.
"Wekeza Kuzuia Ukatili wa Kijinsia". Mgeni rasmi alikuwa Dkt. Gwajima D , Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Siku 16 za Kupinga Ukatili Wa Kijinsia ni Kampeni ya Kimataifa inayoadhimishwa kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 (Siku ya Haki za Binadamu) kila Mwaka ili kuongeza wito wa kutokomeza aina zote za Ukatili wa Kijinsia
Ukatili mwingi dhidi ya Wanawake/Wasichana unafanywa na Watu wa karibu ikiwemo Wenza wao au Wenza walioachana nao.
Kauli mbiu
Wekeza: Kuzuia Ukatili wa Kijinsia, Kauli mbiu hii ni wito kwa kila mmoja wetu kutumia nafasi aliyonayo katika familia, jamii ama taasisi kuchukua hatua thabiti kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia. Kaulimbiu hii pia inasisitiza jamii, taasisi za umma na za binafsi kuwa na hatua za makusudi za kuongeza ulinzi kwa wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia. Wito huu pia unasisitiza ya kwamba vitendo vya ukatili vinazuilika na kinga ni bora kuliko tiba.
CHIMBUKO
Chimbuko la Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati dhidi ya Ukatli wa Kijinsia ni vuguvugu la Wanaharakati Duniani kuelewesha Umma kuhusu uwepo mkubwa wa Ukatili Wa Kijinsia na kukemea Vitendo hivyo
Mauaji ya Kinyama yaliyofanyika Nchini Dominica dhidi ya Wasichana Watatu wa Familia moja (Mirabell Sisters) wakiwa wanatetea Haki za Binadamu yalipeleka Umoja wa Mataifa kutenga Siku hii tangu Novemba 25, 1991 kuwa Siku ya kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake.
Siku 16 za kampeni
Ndani ya Siku 16 za Kampeni ya kupinga Ukatili Wa Kijinsia kuna Siku nyingine za Kimataifa za Haki Za Binadamu ambazo ni pamoja na Novemba 29 ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Watetezi wa Haki za Binadamu Wanawake, Desemba 1 Siku ya UKIMWI Duniani, Desemba 3 Siku ya Watu wenye Ulemavu
Desemba 6 Siku ya kukumbuka mauaji ya kikatili ya Montreal Canada ya Mwaka 1989 ambapo Wanawake 14 waliokuwa wanasomea Uhandisi waliuawa na Mtu aliyekuwa anawachukia Wanawake na Desemba 10 Siku ya Tamko Rasmi la Haki za Binadamu
Siku hizi 16 zinatoa mwanga na msukumo kwa Watu, Serikali, Jamii na Watu binafsi kutambua kwamba ukatili dhidi ya Wanawake ni ukiukwaji wa Haki za Binadamu.
Ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike bado ni mojawapo ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshamiri na kudumu ulimwenguni. Licha ya nchi nyingi kupitisha sheria za kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, utekelezaji dhaifu na mila za kijamii zenye ubaguzi bado ni matatizo makubwa. Kwa kulinganisha kimataifa, wanawake wapatao milioni 736 - karibu mmoja kati ya watatu - wameshuhudia ukatili wa kimwili na/au wa kingono kutoka kwa wenzi wao, ukatili wa kingono usiohusiana na uhusiano wa kimapenzi, au vyote hivyo, angalau mara moja katika maisha yao.
Ukatili dhidi ya wanawake umekuwa mkubwa katika mazingira mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sehemu za kazi na nafasi za mtandaoni. Utafiti wa kimataifa uliofanywa na Economist Intelligence Unit uligundua kwamba asilimia 38 ya wanawake wameshawahi kupata uzoefu wa ukatili mtandaoni, na asilimia 85 ya wanawake wanaotumia muda wao mtandaoni wameshuhudia ukatili wa kidigitali dhidi ya wanawake wenzao.
Utafiti mwingine uliofanywa kimataifa kuhusu wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya teknolojia ulibaini kwamba asilimia 44 ya wanawake waanzilishi walipata aina fulani ya unyanyasaji kazini mwaka 2020, ambapo asilimia 41 ya wanawake walipata unyanyasaji wa kijinsia.
Zaidi ya hayo, janga la COVID-19, mizozo, na mabadiliko ya hali ya hewa vimeongeza zaidi Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike (VAWG), vikichochea changamoto zilizokuwepo awali na kuzalisha vitisho vipya na vinavyojitokeza. Kutokuwa na uhakika wa kiuchumi, maisha yaliyosambaratika, na ulinzi wa kijamii uliopunguzwa bado unaendelea kuongeza uwezekano wa wanawake na wasichana kukumbwa na ukatili.
Ukatili unavyoathiri afya na ustawi wa kimwili na kiakili wa wanawake kwa kila hatua ya maisha yao na kuathiri maendeleo yao kitaalamu na uwezeshaji kiuchumi. Ukatili dhidi ya wanawake pia una matokeo makubwa kijamii na kiuchumi kwa familia, jamii, na jamii nzima, na kuzuia kufikia maendeleo endelevu.
Utafiti mpya wa IMF katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara unaonyesha jinsi ukatili dhidi ya wanawake na wasichana unavyohatarisha maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo. Ongezeko la ukatili dhidi ya wanawake kwa asilimia 1 linahusishwa na kupungua kwa asilimia 9 katika shughuli za kiuchumi.

HALI YA UKATILI WA KIJINSIA NCHINI TANZANIA
Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa hali ya idadi ya Watu na Afya, 2022 (Tanzania Demographic Health Survey, 2022) inaonyesha kuwa 27% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 wamekumbwa na vitendo vya ukatili wa kimwili kuanzia walipokuwa na miaka 15 huku 21% wakiwa wamewahi kukumbana na vitendo vya ukatili wa kingono. Kwa upande wa ukatili majumbani, 39% ya wanawake waneripoti kukumbana na vitendo vya ukatili kutoka kwa wenza wao wa sasa ama waliopita. Pia ripoti inaonyesha vitendo vya ukeketaji ni 8%
Uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kiasi kikubwa unachangiwa na mfumo dume na kukosekana kwa uangalifu wa mgawanyo wa majukumu ya kijamii baina ya wanawake na wanaume. Hali hii pia hupelekea wanawake kushindwa kushiriki katika fursa mbalimbali kama vile za kiuchumi na uongozi na kuchochea zaidi ukandamizwaji.
Umasikini pia, hutajwa kuchochea vitendo vya ukatili wa kijinsia mathalani vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni.

Comments
Post a Comment