SHOO KUBWA YA MAONESHO YA VICHEKESHO VYA WIMA (STAND UP COMEDY) KUWAHI KUTOKEA, DAS WILAYA YA MBEA AKEMEA MASHOGA.

    Ikiwa ni msimu wa pili wa Mbeya Comedy Festival, ni Tar 24November. 2023 ambapo Show hiyo kubwa iliyokuwa imesubiriwa na wakazi wa Mbeya na nje ya mipaka yake kwa takribani miezi mitatu. Hatimaye imeweza kufikia kilele hapo jana Tar 24Nov, Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa Tughimbe Hall. Huwezi kutokuiweka kwenye miongoni mwa Show kubwa kuwahi kufanyika nyanda za juu kusini, hasa Mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
    Mgeni rasmi alikuwa Mh. Dkt Tulia Ackson ambaye ni Mkurugenzi wa Tulia Trust, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Spika wa Bubge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa IPU. Japo kutokana na majukumu aliweza kumtuma Muwakilishi DED wa Wilaya ya Mbeya, ambaye wakati wa kutoa salamu aliweza kuwaasa vijana juu ya nafasi ya kujiwekeza.
"Kwa miaka 10 iliyopita huko nyuma, kumpata shoga ilikuwa ni vigumu saana. Lakini sasa hivi vijana kwakuwa hawataki kufanya kazi za mapambano, wala kujituma ili kupata fula za kujikwamua kiuchumi. Wameamua kujibadili tabia na kuwa tayari kuwa mashoga, ili mradi tu waweze kupata vitonga na kuamini maisha yanakuwa rahisi kwa namna hiyo. Jambo ambalo sio kweli, zaidi tu wanaharibikiwa na maisha yanaharibika kabisa. Nitoe rai kwa vijana, Serikali ya awamu ya sita imetoa mwanya mpana wa kila kijana anaefanya harakati za halali kuwezeshwa. Kila kijana anaweza kuanzisha jambo/biashara yake mahali popote, na akafanikiwa. Pia Mbeya imekuwa Mkoa wenye bahati kupata mtu bingwa kama Dkt. Tulia Ackson, kwasababu ametoa fulsa nyingi kwa vijana tunatakiwa kuzichangamkia. Niwapongeze saana waandaaji wa Mbeya Comedy Festival, pia nadhani ifike wakati vijana kuiga mfano huu ili kuweza kujitengenezea vipato na kuachana na tabia mbovu." DAS Wilaya ya Mbeya.

Mdau "Kiukweli show ilikua poa sana na mlitutendea haki katika kila idara comedian walijua nini wanatakiwa kukifanya, kwa sisi wageni waalikwa haki tulitendewa kwa kiasi kikubwa sana na kama kuna mapungufu basi ni sehemu ya kazi lakini kwa mimi hapa kitu kilicho nileta uko nilifaidika nacho na nili enjoy sana. Nilitamani hata muda ugande cz time ilivyo zidi kwenda ndo burudani ilikua 🔥🔥🔥 ombi langu ni kwamba tuandalieni show nyingne mwezi wa 12 tunavyo kua tunamaliza mwaka itakua poa sana ni hayo tu 🙏"
  SHUKURANI KUTOKA KWA MKURUGENZI WA MBEYA COMEDY FESTIVAL 

 
"Mmetuongezea nguvu ya kupambana na kuhakikisha mnapata kile kilichobora muda wote✊ Nyie ni watu wa muhimu sana kwetu Hakika Tuna deni kubwa la kuhakikisha  Mnapata furaha na kupata kile killichobora Asante kwa kuja TUKUTANE DECEMBER🙏" Stewart ( Mbeya Boy )

Na Wamzi Hassan

Comments

Popular posts from this blog

DKT. TULIA ALIVYO WEZESHA MASOMO KWA VIJANA WANAOTOKA MAZINGIRA MAGUMU MBEYA, SONGWE NA RUVUMA.

RAIS WA IPU MH. DKT. TULIA NA RAIS WA HUNGARY WAJADILI HALI YA AMANI DUNIANI

TK MOVEMENT YAZINDULIWA DODOMA MEI 25,2024, WAZIRI NDEJEMBI AWAAGIZA WATENDAJI KUTOA USHIRIKIANO KWA VIJANA