YAJUE MALENGO 10 YA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII (SMAUJATA) TANZANIA
🇹🇿
DIRA YA SMAUJATA
Kuwa na Taifa lenye Kizazi Huru chenye haki na Usawa Kitakachoweza Kujitegemea kwa Kuzitambua Fursa na Kutumia Ujuzi, Maarifa na Vipaji katika Kujenga Jamii yenye Maendeleo Endelevu.
*DHAMIRA YA SMAUJATA :*
Kuiwezesha na kuijengea Jamii Uwezo wa Kutambua na Kuiishi Misingi ya Haki na Usawa ili Kwa Kutumia Ujuzi, maarifa na Vipaji iweze Kung'amua na Kuzitumia fursa Kuleta Maendeleo Endelevu.
*IMANI YETU MASHUJAA SMAUJATA*
HEKIMA NA UMOJA, USHINDI NA USHUJAA💪🏾👨👩👧👦✊🏿
"Kafanyeni Kazi Kwa Weledi, Ushirikiano na Kwa Kujituma Kila Mmoja Katika Eneo Lake Kazi Ionekane mashujaa.. Baraka Zote Nawapa Mashujaa wa Jamii🤲🏾"
~Sospeter Mosewe Bulugu,
Mwenyekiti SMAUJATA Taifa
🇹🇿
MALENGO MAKUU YA SMAUJATA
1. Kushirikisha Jamii katika kuainisha fursa na changamoto
zinazoikabili ili kulijiletea Maendeleo
2. Kuelimisha Jamii kuondokana na Fikra, Imani, Mila, Desturi
na Tamaduni Zinazokinzana na Maendeleo
3. Kushirikisha Jamii katika Kuiunganisha na Kuiwezesha katika Mchakato wa Maendeleo ili
kuinua ustawi wake.
4. Kuratibu Utekelezaji na Uzingatiaji wa Masuala ya Jinsia
Katika Programu na Mipango ya Maendeleo Katika Sekta
Mbalimbali
5. Kuwezesha Jamii Kutumia Fursa ya Sera za Kisekta na
Mikakati yake katika Kujiletea Maendeleo.
6. Kutoa Elimu Kwa Jamii Kupitia Semina, sanaa, Warsha , Makongamano, Vyombo vya Habari, Matembezi ya Amani , Vipeperushi Kuhusu Haki, usawa, Fursa na Sera mbadala kwa Maendeleo Endelevu na Kuiwezesha Jamii Kutekeleza Haki na Malezi ya Mtoto
7. Kuibua, Kuendeleza na Kukuza Vipaji Mbalimbali katika Ujuzi, Utaalamu na Ubunifu ili Kujenga Kizazi chenye Uwezo wa Kujitegemea.
8. Kushirikiana na Serikali, Wananchi, Wadau mbalimbali Kutoka Ndani na nje ya Nchi katika Shughuli za Utoaji wa Elimu na Fursa za Maendeleo.
9. Kupokea Mbinu wezeshi, Maoni na Mawazo Mapya kutoka Makundi mbalimbali ya Wadau na Kuishauri Jamii na Serikali katika Kuboresha na Kufanikisha Vipaumbele vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
10. Kufanya Shughuli zingine Zozote zinazohusu Maendeleo na Ustawi wa Jamii.
Na Wamzi Hassan
Comments
Post a Comment