TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MIFUKO 50 YA SARUJI SHULE YA MSINGI IKULE MASEBE RUNGWE

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust imetoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji kwa shule ya Msingi Ikule Kata ya Masebe Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kwa ajili ya kukarabati ofisi ya walimu ambapo kwa sasa wanatumia moja ya darasa kama ofisi. Msaada huo umekabidhiwa na Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tulia Trust Dkt Tulia Ackson. Mwakanolo amesema Taasisi ilipokea maombi kutoka uongozi wa shule hiyo hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu Taasisi imewiwa kutoa msaada huo Ili kuchochea ubora wa elimu sanjari na kuungana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu. Innocent Atilyo ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema sehemu kubwa ya shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi ikiwa na madarasa saba na jumla ya watoto zaidi ya mia mbili thelathini ambapo Serikali imetoa milioni thelathini na tano n...