Posts

Showing posts from December, 2023

YAJUE MALENGO 10 YA SHUJAA WA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII (SMAUJATA) TANZANIA

Image
🇹🇿 DIRA YA SMAUJATA Kuwa na Taifa lenye Kizazi Huru chenye haki na Usawa Kitakachoweza Kujitegemea kwa Kuzitambua Fursa na Kutumia Ujuzi, Maarifa na Vipaji katika Kujenga Jamii yenye Maendeleo Endelevu. *DHAMIRA YA SMAUJATA :* Kuiwezesha na kuijengea Jamii Uwezo wa Kutambua na Kuiishi  Misingi ya Haki na Usawa ili Kwa Kutumia Ujuzi, maarifa na Vipaji iweze Kung'amua na Kuzitumia fursa Kuleta Maendeleo Endelevu. *IMANI YETU MASHUJAA SMAUJATA* HEKIMA NA UMOJA, USHINDI NA USHUJAA💪🏾👨‍👩‍👧‍👦✊🏿 "Kafanyeni Kazi Kwa Weledi, Ushirikiano na Kwa Kujituma Kila Mmoja Katika Eneo Lake Kazi Ionekane mashujaa.. Baraka Zote Nawapa Mashujaa wa Jamii🤲🏾"  ~Sospeter Mosewe Bulugu,  Mwenyekiti SMAUJATA Taifa 🇹🇿 MALENGO MAKUU YA SMAUJATA 1. Kushirikisha Jamii katika kuainisha fursa na changamoto  zinazoikabili ili kulijiletea Maendeleo 2. Kuelimisha Jamii kuondokana na Fikra, Imani, Mila, Desturi  na Tamaduni Zinazokinzana na Maendeleo 3. Kushirikisha Jamii kat...

MANYARA: RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN AMESEMA MSIBA HUU NI MSIBA WA TAIFA ZIMA.

Image
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo December 07,2023 ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko katika Mji wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kuongea na Wananchi wa Katesh ambapo amewapa pole na kuwatia moyo kuwa msiba uliotokea ni wa Taifa na sio wa Manyara pekee yao huku akiwahakikishia kuwa Serikali ipo pamoja nao. Rais Samia amenukuliwa akisema “Ni kazi ya Mungu na hatujui Mungu katuletea hili kwa makusudi gani, kwetu sisi ni kupokea na kumshukuru hatuwezi kumlaumu na hili sio letu pekee yetu mwaka jana au mwaka juzi lilitokea Malawi tukaenda kuwasaidia nimekwenda hali ni kama hii utafikiri hakukuwa na nyumba kabisa na ni eneo kubwa, ni kushukuru na kuchukua tahadhari, sasa maeneo ya maji tuyapishe maji yachukue nafasi yake sisi tukae pembeni” “Poleni sana kwa tukio, nimeona nije nione mwenyewe toka juzi mambo yametokea nilikuwa safari mlisikia lakini Waziri Mkuu mara moja na Serikali yote ilikuwa hapa nikawapa maelekezo nini cha kufanya wamejitah...

SERIKALI YACHUKUA HATUA ZA AWALI KUKABILI MAAFA HANANG MKOANI MANYARA

Image
Manyara; Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imechukua hatua za haraka kwa wahanga wa maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope yaliyotokea tarehe 03 Disemba, 2023 ambapo yalitoka mlima Hanang uliopo Mkoa wa Manyara na kusababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu mbalimbali yakiwemo mashamba, na makazi ya wananchi wa eneo hilo. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wamefika katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara eneo yalipotokea maporomoko ya tope Leo tarehe 04 Disemba 2023. Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara Mhe. Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha Gendabi ambalo ni eneo liliothirika Maporomoko ya tope kutoka Mlima wa Hanan...