UKATILI MAJUMBANI
(Pia hujulikana kama unyanyasaji wa nyumbani au unyanyasaji wa kifamilia)
Ni unyanyasaji unaotokea katika mazingira ya nyumbani, kama vile katika ndoa au watu wanaoishi pamoja. Hufanywa na mmoja wa watu katika uhusiano wa karibu dhidi ya mtu mwingine, na unaweza kutokea katika uhusiano kati ya wenzi wa zamani au wenzi wanaoishi pamoja.
Katika maana pana zaidi, unyanyasaji wa majumbani unahusisha pia ukatili dhidi ya
👉🏾Watoto,
👉🏾Wazazi, au
👉🏾Wazee.
Unaweza kuchukua aina nyingi, ikiwa ni pamoja na;
👉🏾Unyanyasaji wa kimwili,
👉🏾Unyanyasaji wa maneno,
👉🏾Unyanyasaji wa kihisia,
👉🏾Unyanyasaji wa kiuchumi,
👉🏾Unyanyasaji wa kidini,
👉🏾Unyanyasaji wa uzazi, au
👉🏾Unyanyasaji wa kijinsia
Nakaribisha maswali na mijadala mbalimbali juu ya maswala ya Ukatili ikiwemo vyanzo na namna ya kupambana dhidi yake
Comments
Post a Comment