MBINGA; MKUU WA WILAYA YA MBINGA AFICHUA UBADHIRIFU WA FEDHA NA VIFAA VYA ZAIDI YA TSHS MILIONI 40 KATIKA UJENZI WA SHULE MSINGI MPYA YA KISASA KIPIKA, KATA YA MATARAWE, HALMASHAURI YA MJI MBINGA, ASISITIZA UADILIFU NI MSINGI IMARA WA MAENDELEO YA TAIFA

      Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Ally Mangosongo pamoja na kamati ya usalama wafichua ubadhirifu mkubwa wa fedha na vifaa vya ujenzi wa shule mpya ya msingi ya mfano kipika, kata ya Matarawe, Halmashauri ya mji wa Mbinga, Ambapo kuna ubadhirifu mkubwa wa fedha na vifaa vyenye thamani ya tshs 35 millioni, ikiwa pamoja na bati 71,mbao 246, na tiles za tshs milioni 25, Hali ambayo imesababisha mradi kutokamilika kwa muda uliopangwa.
Ambapo mradi wa ujenzi huo ulitengewa tshs milioni 331,600,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa jengo moja la utawala, vyoo, majengo matatu ya madarasa na jengo moja la mfano la darasa la awali ili wanafunzi wa maeneo hayo waweze kupata elimu karibu. Ambapo baadhi ya madarasa hayajafungwa  milango, madirisha na kuwekwa malumalu.

Baada ya ukaguzi na uchunguzi wa kina wa nyaraka na taarifa za mradi Mkuu wa Wilaya alisema " Haiwezekani serikali inatoa fedha za miradi alafu wanaibuka watu wachache mno wasiopenda maendeleo wanahujumu, Hivyo basi natoa agizo kukamatwa kwa wale wote waliohusika na ubadhirifu huo kwa uchunguzi kisha hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho kwa watu wengine".
Aidha, Mhe. Mangosongo, Mkuu wa Wilaya alitoa agizo kwa Wahandisi na wasimamizi kutekeleza miradi kwa kuzingatia maelezo ya Bill of Quantities (BOQ) na sio kwa kuzingatia utashi wao, Pia aliwataka mafundi kuzingatia ubora wa kazi sambamba na kuwa waaminifu, ili wapate miradi mara kwa mara, Alikadhalika aliwataka wasimamizi wa miradi kutekeleza maagizo ya viongozi pindi yanapotelewa.

Sambamba na hilo aliwataka wananchi kutoa taarifa za ubadhirifu na kufichua viashiria vya wizi kwenye miradi, Vilevile alitoa siku mbili kwa mafundi wote wanaotekeleza miradi hiyo kufanya marekebisho ya changamoto ambazo zimeainishwa, kujengwa kwa miundombinu ya watu wenye ulemavu pamoja na mafundi kufanya kazi kwa kuzingatia ubora na thamani halisi ya fedha zinatolewa na serikali.

Hata hivyo,Mhe.Mangosongo, alimalizia ziara kwa kukagua ujenzi unaoendelea wa shule ya sekondari mpya ya kisasa Matarawe ambao utagharimu  zaidi ya Tshs milioni 500, kutoka serikali kuu, Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha kitelea ambao upo katika hatua za mwisho kukamilika, Kisha ametembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha kyeju's coffee kuona maendeleo ya kiwanda hicho kwasasa.

Mwisho, Alitoa maagizo kwa halmashauri kwa kipindi cha mwezi mmoja kukamilisha ujenzi wa zahanati kijiji kitelea ili ianze kuhudumia wananchi, Pia alimtaka mmiliki wa kiwanda cha kyeju's coffee kufuata sheria zote za uendeshaji wa kiwanda sambamba na kutoa kipaumbele cha ajira za kazi kwa wazawa wa maeneo hayo ili wanufaike na kiwanda hicho.

       

Comments

Popular posts from this blog

RAIS WA IPU MH. DKT. TULIA NA RAIS WA HUNGARY WAJADILI HALI YA AMANI DUNIANI

TK MOVEMENT YAZINDULIWA DODOMA MEI 25,2024, WAZIRI NDEJEMBI AWAAGIZA WATENDAJI KUTOA USHIRIKIANO KWA VIJANA

TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MIFUKO 50 YA SARUJI SHULE YA MSINGI IKULE MASEBE RUNGWE