Posts

Showing posts from October, 2024

TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MIFUKO 50 YA SARUJI SHULE YA MSINGI IKULE MASEBE RUNGWE

Image
  Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust imetoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji kwa shule ya Msingi Ikule Kata ya Masebe Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kwa ajili ya kukarabati ofisi ya walimu ambapo kwa sasa wanatumia moja ya darasa kama ofisi. Msaada huo umekabidhiwa na Afisa Habari wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tulia Trust Dkt Tulia Ackson. Mwakanolo amesema Taasisi ilipokea maombi kutoka uongozi wa shule hiyo hivyo kwa kutambua umuhimu wa elimu Taasisi imewiwa kutoa msaada huo Ili kuchochea ubora wa elimu sanjari na kuungana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu. Innocent Atilyo ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amesema sehemu kubwa ya shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi ikiwa na madarasa saba na jumla ya watoto zaidi ya mia mbili thelathini ambapo Serikali imetoa milioni thelathini na tano n...

RAIS WA IPU MH. DKT. TULIA NA RAIS WA HUNGARY WAJADILI HALI YA AMANI DUNIANI

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 8 Oktoba, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Hungary, Mhe. Tamas Sulyok katika Ikulu ya nchi hiyo iliyopo Jijini Budapest. Katika mazungumzo yao, Viongozi hao walijadili njia bora za kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa haya mawili, Tanzania na Hungary, katika sekta mbalimbali hususani kilimo, utalii, biashara na maji. Rais Sulyok alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia kwa juhudi zake za dhati katika kuendeleza amani duniani, hususani katika maeneo yanayokumbwa na migogoro mikubwa. Aidha, walizungumzia pia masuala yanayohusu misingi na malengo ya IPU, ambapo Mhe. Sulyok aliahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza ajenda zote za IPU. Ifahamike kuwa kati ya nchi nane zilizounga mkono kuanzishwa kwa IPU katika mkutano uliofanyika tarehe 29 na 30 Juni 1889 nchini Ufaransa, Hungary ilikuwa miongoni mwa...