KUOGA KILA MARA SIO AFYA, OGA MARA MBILI KWA WIKI
Daktari bingwa wa tiba ya uzuwiaji wa magonjwa James Hamblin alifanya utafiti kuhusu utakatishaji wa ngozi ambao hivi karibuni umechapishwa katika kitabu. "Ninajihisi vizuri kabisa ,"alijibu dokta James Hamblin alipoulizwa anajihisi vipi baada ya kuishi bila kuoga kwa kipindi cha miaka mitano. " Unazowea tu", Hamblin ana umri wa miaka 37, na ni mtaalamu aliyesomea taaluma yake katika Chu kikuu cha Yale University kitengo cha huduma ya afya ya umma na ni daktari bingwa wa tiba ya kuzuia magonjwa. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Hamblin hatahivyo anasisitizia juu ya umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni lakini anasema sio lazima kuosha sehemu nyingine za mwili mara kwa mara Ni mmoja wa waandishi wa jarida la Marekani -The Atlantic , ambamo aliandika taarifa iliyokuwa na kichwa cha habari kinachosema :Niliacha kuoga , na maisha yangu yameendelea vyema. "Tunatumia miaka muda wa miaka miwili maishani mwetu kwa kuoga tu. Muda huo unaweza kuzalish...